Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga amesema kuwa Kamati ya Sera ya Fedha ya Bodi ya Benki Kuu ya Tanzania iliyokutana Mei 8 mwaka huu imepitisha hatua mbalimbali za kisera zinazolenga kukabiliana na athari za mlipuko wa Ugonjwa wa homa ya virusi vya Corona COVID-19 katika Uchumi lengo la hatua hizo likiwa kudumisha udhibiti wa sekta ya fedha na upatikanaji wa huduma za fedha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Gavana Luoga amesema Kamati hiyo katika sera hizo imekubaliana Benki kushusha kiwango cha chini cha kisheria cha sehemu ya Amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu ya Tanzania kutoka asilimia 7 hadi 6 kuanzia Juni 8 mwaka huu huku ikitarajiwa kuongeza ukwasi katika Sekta ya Benki.
Aidha Benki Kuu kushusha kiwango cha riba kinachotozwa kwa benki kukopa benki kuu kutoka asilimia 7 hadi asilimia 5 kuanzia Mei 12 mwaka huu hatua itakayowezesha kuongeza wigo wa benki kukopa kutoka Benki Kuu kwa riba nafuu na hivyo kupunguza riba ya mikopo kwa wateja.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment