Polisi imewakamata kiasi wanaharakati 12 wa vuguvugu la maandamano ya mjini Hong Kong katika jimbo hilo maalum la China na kuwapeleka katika jela tofauti, kwa mujibu wa ripoti ya vyombo vya habari jana.
Mhamasishaji maarufu Joshua Wong aliandika katika ukurasa wa Tweeter akiweka na picha, akisema wabunge wa sasa pamoja na wa zamani ni miongoni mwa waliokamatwa.
Gazeti la South China Morning Post, likinukuu duru za mahakama , limeandika kwamba wale waliokamatwa ni pamoja na wabunge wa zamani Martin Lee, Albert Ho, Lee Cheuk-yan, Leung Kwok-hung na Au Nok-hin.
Maafisa pia walifika nyumbani kwa tajiri mkubwa wa vyombo vya habari Jimmy Lai Chee-ying, lakini mmiliki huyo wa gazeti la Apple Daily hakuwapo nyumbani, gazeti hilo liliripoti.
Yeung Sum wa chama cha Democratic na Cyd Ho wa chama cha Labour pia wamekamatwa, limeripoti Hong Kong Free Press, likinukuu chama cha League of Social Democrats katika jimbo hilo.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment