Ubalozi wa Uturuki nchini Uganda na shirika la TİKA umetoa msaada kwa watu wasiojiweza nchini Uganda.
Katika juhudi za kukabiliana na virusi vya corona katika kipindi cha mwezi Mtukufu, ubalozi wa Uturuki mjini Kampala nchini Uganda kwa ushirikiano na shirika la TİKA, shirika ambalo hutoa misaada katika matukio ya dharura imetoa msaada wachakula kwa familia 1 000 nchini Uganda.
Balozi wa Uturuki mjini Kampala Fikret Kerem Alp na mkurugenzi wa TİKA Yahya Acun wametoa msaada wa unga, sukari na maharagwe kwa familia 1 000 baada ya kumkabidhi kiongozi Mary Karoro Okurut.
Balozi wa Uturuki amesema kuwa Uturuki itaendelea kushirikiana na Uganda katika sekta tofauti ikiwemo sekta ya afya.

No comments:
Post a Comment