Search This Blog

Wednesday, April 15, 2020

Trump: Marekani imefikia kilele cha maambukizi’ mapya ya corona


Rais Donald Trump amesema kuwa Marekani "imefikia kilele" cha visa vya ugonjwa mpya wa Covid-19 na kutabiri kuwa baadhi ya majimbo yataondoa marufuku ya kutotoka nje na kurejea katika hali ya kawaida mwezi huu.

Katika maelezo take ya kila siku White House kuhusu ugonjwa huo, Bw Trump amesema muongozo mpya wa kurejelea shughuli za kawaida utatangazwa siku ya Alhamisi baada ya kuzungumza na magavana.

"Tutarejelea hali ya kawaida wanangu, tena sisi sote," rais alisema. "Twataka nchi yetu tena."

Marekani in a zaikai ya watu 638,000 waliothibitishwa kuwa ugonjwa wa Covid-19 na zaidi ya vifo 30,800.

""Takwimu za kitaifa zinaashiria, tumepita kilele cha maambukizi mapya ya virus vya corona," Bw Trump aliwaambia waandishi wa habari Rose Garden siku ya Jumatano.

"Ni matumaini yangu tutaendelea hivyo, na tutaendelea kufanya kupiga hatua zaidi''

Alipoulizwa Marekani ina idadi kubwa ya watu 136,908, waliofariki katakana na ugonjwa huo kote duniani, Bw Trump alilaumu baadhi ya mataifa kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu idadi ya vifo.

"Kuna mtu anaamini idadi ya vifo vya baadhi ya nchi?" alisema, na kutaja China.

Pia alisema Marekani inachunguza madai kuwa virusi vya corona vilikuzwa ndani ya maabara mjini Wuhan na kwamba chanzo chake sio soko la mji huo.

Vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa ubalozi wa nchi hiyo mjini Beijing unahoji usalama wa maabara mbili iliyopo Wuhan.

Hatahivyo siku ya Jumanne Jenerali Mark Milley, mwenyekiti wa pamoja wa wakuu watumishi wa umma, alisema idara ya ujasusi wa Marekani inaamini huenda janga la corona 'sio jana la kawaida'.

Utawala wa Trump uliwahi kusema kuwa Mei mosi ndio tarehe ambayo taifa hilo huenda ikarejelea hali yake ya kawaida, lakini rais alisema baadhi ya majimbo huenda yakafanya hivyo kabla ya wakati huo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...