Search This Blog

Tuesday, April 7, 2020

Treni zageuzwa kuwa hospitali za uangalizi India

Nchi ya India imesitisha safari za usafiri wa treni kupitia Shirika lake la Indian Railways, badala yake watatumia kama hospitali za muda kwa ajili ya uangalizi na matibabu ya mlipuko wa ugonjwa wa Virusi vya Corona.

Shirika la reli nchini India linashika nafasi ya nne kati ya mashirika makubwa ya usafiri huo duniani na kwa mara ya kwanza wametangaza kufunga kufanya shughuli hizo baada ya kupita miaka 167.


Waziri Mkuu wa Taifa hilo Narendra Modi, alitangaza watu kutotoka nje siku ya Machi 25 na shirika hilo lilipewa muda wa kusafirisha abiria wanaotumia usafiri huo hadi Aprili 14, ila wamesitisha kutokana na ugonjwa huo kusambaa kwa wingi nchini humo.

April 1 nchi ya India iliweka rekodi ya kutangaza kesi 4,288 ya Virusi vya ugonjwa wa Corona na vifo 117 vya ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...