Search This Blog

Thursday, April 23, 2020

Ndanda FC kinara utovu wa nidhamu

By Yohana Challe, Mwananchi yohana.chance@gmail.com

Dar es Salaam. Ndanda inaongoza kwa wachezaji wake kupewa kadi nyekundu na njano katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Wakati ligi ikiwa imesimama baada ya michezo 285 kuchezwa ikiwa ni mzunguko wa 28, kadi nyekundu 28 na njano 747 zimetolewa.

Pia rekodi inaonyesha mabao 566 yamefungwa katika mechi za ligi hiyo yenye timu 20 za Tanzania Bara.

Ndanda ina kadi nne nyekundu na njano 50. Omari Ramadhani, Kiggi Makasi, Hemedi Koja, Samson Mbangula na Adil Buha walipewa kadi nyekundu.

Lipuli ni David Kameta, Joshua Ibrahim, Peter Mapunda, Haroun Mandanda (Mbeya City) na Makyada Makolo wa Mbao.

Timu zenye kadi moja nyekundu ni Azam (Shaban Chilunda), Polisi Tanzania (Yasin Salum), JKT Tanzania (Kelvin Nashon) na Namungo yuko Karlos Kirenge.

Advertisement

Timu ambazo hazina kadi nyekundu ni Simba ingawa ina njano 25, Biashara United (48), Coastal Union (30), Kagera Sugar (34), Mwadui, KMC na Ruvu Shooting (37).

Makolo alipewa kadi nyekundu mara mbili, Koja za njano tisa akifuatiwa na Sylivester Chitembe wa Mbao mwenye kadi za njano nane.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...