
Dar es Salaam. Kocha wa Yanga, Luc Eymael ameamua kukata mzizi wa fitna kwa makipa wake baada ya kuweka wazi siri ya kumpa nafasi Metacha Mnata katika kikosi chake.
Metacha aliyesajiliwa na Yanga msimu huu akitokea Mbao amekuwa na kiwango kikubwa mbele ya makipa wenzake, Faroukh Shikhalo na Ramadhani Kabwili.
Eymael aliliambia Mwananchi makipa wote wazuri lakini kiwango ambacho anakionyesha Metacha ndio kimemfanya apate nafasi mara kwa mara.
“Metacha yupo katika timu ya Taifa hilo kila mmoja analijua, tumekuwa na ratiba ngumu lakini bado anafanya vizuri,” alisema.
Kocha huyo alifunguka zaidi na kusema ni ngumu kubadili makipa wakati yupo ambaye ana kiwango cha kumvutia na anafanya vyema uwanjani.
No comments:
Post a Comment