Search This Blog

Wednesday, April 8, 2020

Mshahara mtamu, Sanchez kasema haondoki Man U

MANCHESTER, ENGLAND . MANCHESTER United mnalo hilo. Kinachoelezwa ni kwamba fowadi wao, Alexis Sanchez ameripotiwa kugoma kushusha mshahara wake ili kuachana na timu hiyo.
Sanchez ameshindwa kuonyesha makali makubwa tangu alipotua Man United akitokea Arsenal, ambapo katika mechi 45 alizocheza, amefunga mabao matano tu.
Msimu huu, Sanchez ameutumikia akiw akwa mkopo huko Inter Milan, mahali ambako amefunga bao moja na kuasisti mara mbili kabla ya muda mwingi kuwa nje ya uwanja kutokana na kuwa majeruhi.
Kwa mujibu wa The Evening Standard, staa huyo wa kimataifa wa Chile amegoma kushuha mshahara wake ili kupata timu itakayomsajili ahame Man United, huku timu hiyo ikifahamu wazi itakuwa kwenye wakati mgumu wa kupata mnunuzi kutokana na mtikisiko wa kiuchumi unaosababishwa na janga la virusi vya corona.
Ripoti hizo zimedai kwamba Sanchez hawezi kubadili msimamo wa kuhusu mshahara, jambo litakalowagharimu Man United zaidi ya Pauni 10.8 milioni kwa mwaka kugharimia mshahara wa mchezaji huyo baada ya Inter Milan kuonekana kwamba hawana mpango wa kumbeba jumla.
West Ham United iliripotiwa kuwasiliana na wakala wa Sanchezo, lakini shida inakuja kwenye mshahara wake, hawana uwezo wa kulipa zaidi ya Pauni 450,000 kwa wiki.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...