Search This Blog

Wednesday, April 8, 2020

Kane azidi kuambiwa aondoke zake Spurs

LONDON, ENGLAND . STRAIKA, Harry Kane ameshauriwa ajifikirie yeye mwenyewe kwanza kabla ya Tottenham Hotspur na kama kutakuwa na timu ya maana wakiwamo Manchester United akileta ofa ya kutaka kumsajili kwenye dirisha lijalo basi afanye haraka kwenda kujiunga nao.
Ushauri huo umetolewa na staa wa zamani wa Spurs, Dimitar Berbatov, ambaye huko nyuma hakusita kuachana na timu hiyo wakati Man United ilipomfuata akakipige Old Trafford, mwaka 2008.
Berbatov alibeba mataji mawili ya Ligi Kuu England katika kipindi cha miaka minne aliyokuwa Man United na anaamini kwamba Kane atatimiza ndoto zake za kubeba mataji kama ataiga kile ambacho yeye alikifanya, alipoondoka Spurs akiwa kwenye kiwango cha juu kisoka.
“Naona kuna mambo mengi yanayofanana hapa, nilipitia kile anachopitia Kane kwa sasa," alisema Kane, ambaye alijiunga na Man United kwa ada ya Pauni 30.75 milioni.
“Naona kabisa anapita kwenye njia zilezile, kipindi ambacho unawaza nipo kwenye kiwango bora na nataka kushinda mataji.”
Man United ni moja ya klabu vigogo huko Ulaya ambavyo vimekuwa zikifukuzia saini ya Kane, ambaye msimu wake ulitibuka Januari baada ya kuumia misuli.
Straika huyo Mwingereza alifunga mabao 27 katika mechi 31 alizochezea klabu yake na timu ya taifa kabla ya kuumia. Mkataba wake umebakiza miaka minne huko Spurs, ambako analipwa Pauni 200,000 kwa wiki, lakini hilo halizizuiii klabu nyingine huko Ulaya kutaka saini yake.
Kane mwenyewe alisema: “Naipenda Spurs, siku sote nitaipenda Spurs, lakini hilo ni jambo moja. Siku zote nimekuwa nikisema siwezi kuhisi mafanikio kama sitaona mwelekeo sahihi na mimi kubaki hapa kwasababu ya mapenzi. Nataka mambo yabadilike, nataka kuwa mmoja wa wachezaji wa daraja la juu. Mambo yabadilike, kinyume cha hilo, siwezi kusema nitabaki hapa milele.”

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...