Search This Blog
Wednesday, April 1, 2020
MOI yapokea viungo bandia vyenye thamani ya Sh 80.9 milioni
Kampuni ya EAA Co. ltd ya nchini Japan imetoa msaada wa viungo bandia vyenye thamani ya shilingi milioni 80.9 kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) leo Aprili Mosi 2020, jijini Dar es Salaam.
Akipokea msaada huo Mkurugenzi wa tiba MOI Dkt Samwel Swai amesema kuwa msaada huo utasaidia kwa kiasi kikubwa matibabu ya wagonjwa wenye ulemavu wa miguu na mikono.
Naye meneja wa kampuni ya EAA C.o Ltd Josiah Benedict amesema ameguswa na changamoto zinazowakabili watanzania ndiyo maana wameamua kuunga jitihada za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt Pombe Magufuli yakuboresha huduma ya afya hapa nchini.
Aidha msaada huyo unatokana na juhudi za Ubalozi wa Tanzania na Japan kwa kushirikiana na watanzania waishio nchini humo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment