KAMA Kuna watu wanadhani Matheo Anthony anajutia kuondoka Yanga watakuwa wamechemka kwani katamka kwamba anaona milango inafunguka tangu ajiunge na Polisi Tanzania.
Alisema tangu ajiunge na Yanga mwaka 2015 hakuwa na namba ndani ya kikosi hicho, kitu kilichokuwa kinampoteza kwenye ramani ya soka.
Alisema kutua kwake Polisi Tanzania amekuwa akipangwa kwenye kikosi cha kwanza na ameanza kurejesha makali yatakayomfanya afike mbali katika kazi hiyo.
“Sijutii kuondoka Yanga kwa sababu nilikuwa sipati nafasi ya kucheza tofauti na Polisi Tanzania naanza kikosi cha kwanza, hivyo inakuwa rahisi kupata taswira ya naenda wapi,” alisema.
“Sina maana kwamba sina cha kukumbuka Yanga, nakumbuka mengi hiyo ni klabu kubwa na nimepata hatua mbalimbali za kimaendeleo,” alisema na kuongeza anatamani kufanya makubwa ili kipaji chake kiweze kuonekana ndani na nje ya nchi.
“Siwezi kusema nitaka kwenda wapi bado ni mapema natakiwa kuendelea kupambana ili kuishi ndoto yangu ya kutamani kufika mbali.”
No comments:
Post a Comment