Search This Blog
Tuesday, April 14, 2020
DC Iringa: Wahudumu wa baa lazima kuvaa barakoa
MKUU wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, ameagiza wamiliki wa baa kuhakikisha wafanyakazi wao wanavaa barakoa kwa ajili ya kujikinga na virusi vya corona.
Aidha, amtaka kila mmiliki wa sehemu zenye mikusanyiko ya watu kuhakikisha kuna maji yanayotiririka na sabuni kwa ajili ya watu kunawa.
Akizungumza na wamiliki wa baa, Mkuu huyo wa wilaya alisema ni muhimu wahudumu hao kuhakikisha wananawa mikono ikiwamo kutumia majitiba.
Aidha, alisema wilaya hiyo imejipanga vyema na iwapo itatokea mtu mwenye maambukizi hatua zitachukuliwa za kumtenga na kuwachukua na kuwatenga na jamii.
Kwa mujibu wa Kasesela, wamiliki hao wanapaswa kuhakikisha wateja na wahuduma wanakaa umbali uliopendekezwa na wizara ikiwa ni hatua ya kujikinga na maambukizi.
“Wale wote wanaokuwa kwenye maeneo ya burudani wanapaswa kukaa kwa umbali unaotakiwa na watakaokiuka watachukuliwa hatua kwa kufunga biashara zao,” alisema.
Kwa kuonyesha mfano, Mkuu huyo wa wilaya ambaye alikuwa amevaa barakoa, alisema ni lazima watu kukaa kwa umbali wa mita moja, ikiwamo wapenzi kuhakikisha wanajitenga.
Kuhusu muda wa kufunga baa, Kasesela alisema Manispaa hiyo itaangalia muda wa kufunga kwa kuwa wapo wanaoendelea kufanyabiashara hadi usiku wa manane.
Aidha, alisema anakusudia kukutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wafanyabiashara mkoani humo kujadili suala hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment