
London, England. Liverpool imeingia katika vita ya kuwania saini ya mshambuliaji wa Paris Saint Germain (PSG) Kylian Mbappe.
Kocha Jurgen Klopp anataka saini ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kujaza nafasi ya Sadio Mane endapo ataondoka Anfield.
Real Madrid imetenga Pauni150 milioni kutaka saini ya Mane katika usajili wa majira ya kiangazi msimu ujao.
Mbappe amekuwa akiwindwa na Real Madrid kwa muda mrefu, lakini PSG imekuwa ikimuwekea ngumu.
Kwa mujibu wa gazeti la Sun, Liverpool ina hofu ya kumpoteza Mane hivyo imeanza kuchukua hatua mapema kusaka mrithi wake na chaguo la kwanza ni Mbappe.
Miezi 18 iliyopita Liverpool ilikubali kumuuza nyota huyo wa Senegal kwa Pauni150 milioni kwa mkataba utakaomalizika mwaka 2023, lakini Real Madrid na wawakilishi wa Mane walishindwa kufikia mwafaka.
Tangu Mane alipojiunga na Liverpool akitokea Southampton kwa Pauni 34 milioni mwaka 2016, amefunga mabao 77 katika mechi 161 alizocheza Liverpool.
No comments:
Post a Comment