Search This Blog

Monday, April 13, 2020

Beki aziingiza vitani Man United, Man City

London, England. Manchester United na Manchester City ziko  tayari kuingia vitani kuwania saini ya beki wa RB Leipzig Dayot Upamecano.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya miaka 21, amekuwa katika kiwango bora.

Makocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer na mwenzake wa Man City Pep Guardiola wamevutiwa na kiwango cha kinda huyo.

Pia miamba mingine Real Madrid na Bayern Munich zimo katika  mbio za kuwania saini ya beki huyo katika usajili wa majira ya kiangazi msimu ujao.

Kinda huyo anatazamwa kuwa atakuwa mmoja wa mabeki bora Ulaya kutokana na kiwango chake msimu huu.

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amewaambia vigogo wa klabu hiyo kusaka saini ya Upamecano.

Advertisement

Mara kadhaa Upamecano amewahi kuonywa na watendaji wa klabu yake ya RB Leipzig wakimtaka kubaki ili kuongeza ubora na kupata uzoefu wa kutosha kabla ya kuondoka.

Arsenal iliwahi kumtupia ndoano Upamecano mapema msimu huu lakini ilishindwa kutoa Pauni72 milioni.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...