shirikisho la soka nchini Italia linatumai kwamba wachezaji wake watafanyiwa vipimo vya virusi vya corona mwanzo wa mwezi Mei ili kujiandaa kuendelea na msimu wa ligi.
Hakuna tarehe maalum iliowekwa kuhusu kuendelea kwa mechi za msimu huu nchini Itali, huku kukiwa na mizunguko 12 na mechi nne ambazo hazijachezwa.
''Mara tu hali itakaporuhusu tutamaliza msimu huu'' , alisema rais wa shirikisho hilo Gabriela Gravina.
Akizungumza na Sky Sports , aliongezea : Hivi karibuni kutakuwa na mkutano tutabaini mipango iliopo ambapo baadaye tutatangaza.
''Tutaanza , natumai, mwanzo wa Mei na vipimo ili kuhakikisha kwamba wachezaji hawana virusi ili mazoezi yaanze''.
"Tutaanza kucheza katika majira ya kiangazi? Hatuna muda maalumu laikini wazo letu ni kumaliza michuano hii."
Italia ni moja ya nchi ambazo zimeathirika zaidi na janga la virusi vya corona, huku wachezaji wa baadhi ya timu wakipata maambukizi.
Klabu ya Juventus inaongoza ligi ya Seria A kwa pointi moja nyuma ya Lazio huku Inter Milan ikiwa nyuma yao kwa pointi tisa.
Wiki iliyopita, timu za Ujerumani zilikuwa za kwanza barani Ulaya kuanza mazoezi huku wakiwa wanachukua tahadhari dhidi ya maambukizi.

No comments:
Post a Comment