Search This Blog
Monday, April 20, 2020
Hospitali ya Muhimbili Yakanusha Madai Kuwa Muuguzi Wake Amefariki Kwa Corona
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imekanusha taarifa zinazosambaa kuwa Muuguzi Evodia Kapinga amefariki kwa #COVID19 na kwamba alikuwa anahudumia Wagonjwa wa #CoronaVirus
Taarifa ya Hospitali hiyo imesema, Muuguzi huyo hajawahi kuhudumia wagonjwa wa #COVID19 ila alikuwa anatoa huduma kliniki ya watoto wenye tatizo la afya ya akili iliyopo jengo la watoto Muhimbili
Pia, taarifa imesema marehemu alikuwa na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua siku nyingi japo kwa maadili ya kazi hawakutaja maradhi hayo
Evodia Kapinga alizidiwa Aprili 18 akiwa nyumbani kwake Kimara na amefariki leo alfajiri, Aprili 19 akiwa hospitali ya Sinza Palestina. Taarifa imesisitiza kuwa uvumi wa kuwa amefariki kwa #CoronaVirus upuuzwe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment