Search This Blog

Sunday, April 12, 2020

Hesabu za Mbeya City kujinasua kushuka

By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Vita ya kujikwamua kushuka daraja inampa changamoto Kocha wa Mbeya City, Amri Said ambaye anapiga hesabu ya kuinusuru timu hiyo kwa kuchukua pointi nane ugenini na 15 nyumbani.

Mbeya City ni ya nne kutoka mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara (TPL) ikiwa na pointi 30 mbele ya Alliance FC yenye pointi 29, Mbao FC ikiwa na pointi 22 na Singida United yenye pointi 15.

Licha ya Ligi kusimama kipindi hiki kwa tahadhari ya ugonjwa wa corona, kocha huyo anasema ili kuinusuru timu hiyo ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya ni kushinda mechi saba kati ya tisa walizobakiza.

“Nikifanikiwa katika hili hatushuki daraja,” alisema kocha huyo ambaye alikabidhiwa kikosi cha Mbeya City kikiwa nafasi ya pili kutoka mwisho kwenye msimamo.

Alisema mikakati aliyonayo ni kushinda mechi zake tano za nyumbani na nne za ugenini ili kuhakikisha kuwa anachukua pointi nane.

“Tutakwenda Mtwara kucheza na Ndanda na Namungo, huko nitapambana kuhakikisha nachukua pointi nne, nishinde mechi moja na moja nitoke sare. Mikakati hiyo tumeiweka pia kwenye kwenye mechi zetu za Dar es Salaam tutakapocheza na KMC na Azam.”

Advertisement

Alisema katika mechi zao za nyumbani hawatarajii kufanya makosa ambayo yatawagharimu kipindi hiki ambacho wako kwenye hatari ya kushuka. “Naamini hesabu zitakubali na Mbeya City itasalia Ligi Kuu msimu ujao kama tukikusanya pointi nane ugenini na 15 nyumbani katika mechi zetu tisa zilizosalia,” alisema.

Akizungumzia harakati zake tangu amekabidhiwa kikosi hicho, mchezaji huyo wa zamani wa Simba alisema Yanga, Azam na KMC ndizo zimemgharimu.

“Tungekuwa katika nafasi nzuri tu katika msimamo, lakini sare ya bao 1-1 na Yanga na ile ya Azam zimetugharimu, tulipata pointi mojamoja, lakini zilikuwa ni mechi za kutupa pointi sita tulifanya uzembe.

“Hata kipigo cha bao 1-0 na KMC nacho kilitokea kwa uzembe tu tena dakika za mwisho, makosa ambayo sitarajii yatokee katika mechi tisa zilizosalia,” alisema.

Kama ligi itaendelea, timu nne zitashuka daraja moja kwa moja msimu huu na mbili zitacheza mtoano (playoff) kutafuta nafasi ya kubaki Ligi Kuu msimu ujao.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...