Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea club ya Chelsea ya England Olivier Giroud ,33, amejibu kejeli za mfaransa mwenzake anayekipiga Real Madrid Karim Benzema kwa kumlingishia mafanikio yake.
Benzema ,32, alikuwa akiulizwa maswali kupitia instagram na ndio akaringanishwa uwezo wake na Olivier Giroud nani mkali akatoa jibu ambalo wengi walitafsiri kama dharau kwa Giroud.
”Huwezi kulinganisha gari la Formula 1 na Go Kart (Magari ya kuchezea watoto) mimi ndio kama hivyo (F1)” Benzema
Baadae Befoot walimtafuta Giroud na kumuuliza kuhusiana na comment ya Benzema juu yake na kutoa jibu la “Mimi ni nani Go kart? (magari ya kuchezea watoto), mimi ni Bingwa wa Dunia”>>> Giroud akijitamba kuwa kachukua World Cup 2018 Benzema akiwa hajawahi.
Benzema aliachwa kuitwa timu ya taifa ya Ufaransa iliyokuwa inafundishwa na kocha Didier Deschamps toka 2015 kutokana na kuwa katika uchunguzi wa kudaiwa kujihusisha na kurekodi (tape) ya ngono.
2018 kuelekea fainali za Kombe la Dunia wengi wakitarajia kuwa Benzema anaweza kuitwa lakini aliachwa na kuitwa Olivier Giroud kitu ambacho kilizua mjadala mzito mtandaoni, Ufaransa ikiwa na Giroud ilishinda Kombe la Dunia licha ya Giroud kumaliza michuano hiyo bil goli.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment