Search This Blog

Monday, April 27, 2020

Dili la Kanda na Simba liko hivi

By CHARLES ABEL

UPO uwezekano mkubwa kwa winga Deo Kanda kuendelea kuichezea Simba msimu ujao, lakini uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kuwa bado dili la mchezaji huyo kuichezea klabu hiyo kwa uhamisho wa moja kwa moja halijakamilika mpaka sasa.

Kanda ameonyesha kiwango bora katika kikosi cha Simba msimu huu licha ya kutokuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza akiichezea kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka TP Mazembe ambako ameshindwa kupata nafasi kutokana na ushindani wa namba uliopo.

Winga huyo mwenye miaka 30 anayeweza pia kucheza kama mshambuliaji na kiungo mshambuliaji, ameifungia Simba mabao sita katika Ligi Kuu huku akianza katika kikosi cha kwanza mara 10 tu.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa aliliambia gazeti hili kuwa winga huyo hadi sasa ni mchezaji halali wa TP Mazembe na ikiwa kuna makubaliano yatakayofikiwa, ufafanuzi utatolewa hapo baadaye.

“Niweke hili wazi kwamba Deo Kanda kwa sasa ni mchezaji wa TP Mazembe hilo naomba lieleweke. Kama kuna jambo lolote litakalofanyika, klabu itatoa taarifa rasmi lakini kwa sasa yupo Simba kwa mkopo,” alisema Mazingisa.

Kauli hiyo ya Mazingisa huenda ikaongeza presha zaidi kwa mashabiki wa Simba juu ya hatma ya winga huyo aliyegeuka kuwa kipenzi chao baada ya kuibuka kwa tetesi kuwa anahitajiwa na Yanga iliyopania kuimarisha kikosi chao.

Advertisement

Hata hivyo, miezi miwili iliyopita, winga huyo alielezea nia yake ya kutaka kuendelea kuitumikia Simba ikiwa itafikia makubaliano na TP Mazembe ya kumsajili moja kwa moja.

“Bado natamani kuendelea kuichezea Simba. Najiona nina deni kwa mashabiki ambao wamekuwa wakinisapoti lakini, pia na uongozi kwa mikakati mizuri waliyonayo,” alinukuliwa Kanda.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...