Search This Blog

Monday, April 13, 2020

Birdman na Toni Braxton kufunga ndoa mwaka huu

Baada ya kuwepo kwa sintofahanu nyingi kwenye mahusiano yao kwa muda mrefu, hatimaye Birdman na Toni Braxton kufunga ndoa mwaka huu.

Kwenye mahojiano ya njia ya simu na kipindi cha "Rick and Sasha", Braxton alitoa taarifa hiyo ambapo alisema licha ya kupitia changamoto nyingi yeye na mchumba wake #Birdman katika maisha yao, hatimaye watafunga ndoa na wamepanga kutofanya harusi kubwa.

Katika kusisitiza ni lini harusi hiyo itafanyika, #Braxton (52) alisema.. "Tumejaribu kupanga, lakini kwa uhakika tutafunga ndoa mwaka huu" alisema Braxton.

Itakumbukwa, wawili hao walianza mahusiano Mei 2016 na kutangaza uchumba wao Februari 2018. Januari 2019 walitangaza kuvunjika kwa uchumba wao, baadaye April 2019 walitangaza tena kuwa bado wapo pamoja.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...