
LONDON, ENGLAND . STRAIKA wa Crystal Palace, Wilfried Zaha ni staa mwingine aliyejitolea kwa vitendo kupambana na mlipuko wa virusi vya corona, baada ya kutoa nyumba zake 50 kusaidia wafanyakazi wa Mamlaka ya Huduma za Afya (NHS).
Zaha ni sehemu ya wawiliki wa kampuni ya ZO Properties, inayotoa makazi wafanyabiashara ambao huwa safarini, lakini sasa kampuni hiyo imemamua kutoa maghorofa yake bure yatumiwe na wafanyakazi wa NHS.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka England, Zaha ametoa majengohayo ili yatumiwe na NHS kuwapa madaktari na manesi watakaohitaji kukaa karibu na hospitali baada ya kutoka kazini.
Inaelezwa kuwa Zaha alimwambia mmiliki mwenzake wa mijengo huyo Obi Williams kuwa wanahitaji kurudisha kitu kwa jamii na hiyo ndiyo njia sahihi ya kufanya hivyo.
Zaha anafuata nyayo za mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich na staa wa zamani wa Manchester United, Gary Neville na Ryan Giggs kutoa sehemu ya bure kwa ajili ya kuwahifadhi watumishi wa afya wanaopambana usiku na mchana kumaliza tatizo hilo nchini England.
No comments:
Post a Comment