Search This Blog
Tuesday, March 24, 2020
Wachezaji wa Bayern Munich, vilabu vingine vya Bundesliga kupunguziwa mishahara
Wachezaji wa kandanda wa timu kubwa za Ujerumani ikiwemo Bayern Munich wamekubali kupunguziwa mishahara yao ili kuvisaidia vilabu vingine kukabiliana na athari za kiuchumi za virusi vya corona.
Gazeti la Bild limeripoti kuwa wachezaji na maafisa wa mabingwa wa Ujerumani Bayern, wamekubali kupunguza mishahara yao kwa asilimia 20.
Wachezaji wa Borussia Moenchengladbach walikuwa wa kwanza katika Bundesliga kupendekeza kupunguziwa mishahara yao, wakifuatiwa na Werder Bremen na Schalke.
Borussia Dortmund na Bayer Leverkusen wanafanya mashauriano na wasimamizi kuhusu mapendekezo ya kupunguza mishahara yao. Kama tu ilivyo kwa ligi kubwa za Ulaya, Bundesliga inapoteza mapato kutokana na matangazo, ufadhili na mauzo ya tiketi wakati huu wa janga la COVID-19, ambapo mechi za ligi Ujeurumani zimesitishwa hadi Aprili 2.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment