Idadi ya vifo vinavyotokana na maambukizi ya virusi vya corona nchini humo inaongezeka kila uchao nchini Italia.
Hadi kufikia jana Jumamosi watu 800 walikufa, na kuifanya idadi jumla kufika karibu watu 5,000 waliokufa kutokana na homa ya COVID 19 nchini humo.
Kufuatia hali hiyo, serikali ya nchi hiyo imeamrisha biashara zote kufungwa hadi ifikapo Aprili 3.
Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte amesema kupitia vidio iliyoruishwa kwenye mtandao wa Facebook kwamba wakati huu ni mbaya kuwahi kutokea tangu baada ya kumalizika vita vya dunia, na kuongeza kwamba shughuli za kibiashara zilizo muhimu ndizo zitaruhusiwa kuendelea kufanya kazi.
Tangu Alhamisi iliyopita, Italia ilichukua nafasi ya kwanza na kuipita China kwa idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya virusi hivyo vya corona.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment