Search This Blog

Thursday, March 19, 2020

Virusi vya Corona: Mkutano wa G7 utafanyika kupitia video

Rais wa Marekani Donald Trump amefuta Mkutano wa viongozi wa mataifa 7 tajiri dunaini G7 na badala yake watazungumza kwa njia ya vidio kutoa fursa kwa viongozi kushughulikia mpripuko wa maambukizi ya virusi vya corona katika nchi zao.

Mkutano huo uliokuwa uwakutanishe viongozi wa mataifa ya Canada, Ufaransa, Ujerumani, Japan, Italia, Uingereza na Marekani ulikuwa ufanyike mnamo mwezi Juni katika jimbo la Marekani la Maryland.

Trump pia atakutana na viongozi wa mataifa hayo saba kwa njia ya video mnamo mwezi Aprili na Mei baada ya viongozi hao kufanya mkutano kuhusu mripuko wa virusi vya corona wiki hii.

Kwa hali inavyoendelea, serikali ya Trump inaamini mripuko wa virusi vya corona utaendelea kuwa na athari ulimwenguni hadi majira ya joto.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...