Search This Blog
Tuesday, March 17, 2020
Umeme wa TANESCO kushusha bei
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu amesema kuwa bei ya umeme itashuka baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere kutokana na gharama nafuu ya uzalishaji umeme kwa maji kuwa nafuu (Shilingi 36 kwa yuniti) ukilinganisha na vyanzo vingine mfano gesi ambayo hugharimu Shilingi 147 kwa yuniti moja.
“Baada ya punguzo la bei ya umeme tunatarajia hata viwandani gharama za uendeshaji zitashuka na hivyo mabadiliko hayo yatakwenda sambamba na kupungua kwa bei ya mali na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa viwandani hapa nchini hivyo kupunguza mfumoko wa bei na kuviwezesha viwanda vyetu kufanya ushindani kimataifa” amesema Naibu Waziri Subira Mgalu
Kwa upande wake Arun Lodhia, ambaye ni mmiliki wa kiwanda cha Lodhia Group kinachozalisha bidhaa za chuma na plastiki amesema, kiwanda chake kinatarajia kupata ahueni kubwa endapo bei ya umeme itapungua na wataweza kushusha bei ya bidhaa zao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment