Search This Blog
Monday, March 30, 2020
Tanzia: Katibu mkuu wa CUF Khalifa Suleiman Khalifa afariki dunia
Katibu Mkuu wa CUF, Khalifa Suleiman Khalifa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Machi 31 2020 katika hospitali ya Aga Khan alikokuwa akipatiwa matibabu.
Akizungunza na Mwananchi, mwanaye Said Khalifa amesema tangu Januari 2020 kwa nyakati tofauti baba yake aliugua na kulazwa katika hospitali hiyo.
"Karibu mara tatu mzee alilazwa Aga Khan akipatiwa matibabu na akipata ahueni tulikuwa tunarudi nyumbani kujisikilizia. Kwa sasa siwezi kuzungumza kwa kirefu nahisi nimechanganyikiwa naomba unitafute baadaye," amesema Said.
Machi 16, 2019 Khalifa akichaguliwa na baraza kuu la uongozi la CUF kuwa katibu mkuu wa pili wa chama hicho akichukua nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alivuliwa uanachama.
Mwili wa Khalifa utazikwa leo katika makaburi ya Kisutu wilayani Ilala, Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment