Search This Blog

Wednesday, March 25, 2020

Spika wa bunge la Israel, mshirika wa Netanyahu ajiuzulu


Spika wa bunge la Israel, ambaye ni mshirika wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, amejiuzulu leo, na kuendeleza mapambano na Mahakama ya Juu nchini humo kuhusu hofu yake kwamba demokrasia huenda ikaathirika kutokana na mgogoro wa virusi vya corona.

Kujiuzulu kwa Yuli Edelstein huenda kukawezesha mipango ya upinzani kuharakisha sheria ambayo itamzuia Netanyahu, kama mshukiwa aliyeshitakiwa katika kesi tatu za ufisadi, kuunda serikali mpya kufuatia uchaguzi wa Israel wa Machi 2.

 Edelstein, mwanachama wa chama cha Netanyahu cha siasa za mrengo wa kulia Likud, ametangaza kuwa anajiuzulu katika hotuba yake kwa bunge, akiituhumu mahakama ya juu kwa ukiukaji mkubwa na uingiliaji wa masuala ya bunge kwa kumuamrisha kuandaa kura ya kumtafuta spika mpya katika kikao cha leo cha bunge la Israel, Knesset.

 Baada ya kutangaza kuwa anajiuzulu, Edelstein akaahirisha vikao vya bunge hadi Jumatatu wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...