Search This Blog

Friday, March 6, 2020

Simba, Yanga ni jino kwa jino miaka 10

By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Wakati nyota wa Simba na Yanga wakitoa mitazamo tofauti kwenda kwenye mechi ya Jumapili ya watani, mshindi wa mechi hiyo ataandika heshima ya kumfunga mara nyingi zaidi mpinzani wake kwa miaka 10 iliyopita.

Simba na Yanga watakutana kwa mara ya pili msimu huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 kwenye mzunguko wa kwanza.

Mashabiki wa timu hizo kila mmoja amekuwa akimtambia mwenzake kuchomoza na ushindi kesho, huku nyota wa zamani wa timu hizo kongwe wakitoa tathimini yao kwenda kwenye mchezo huo wa watani wa jadi.

Licha ya tambo za kila upande, rekodi za miaka 10 za timu hizo zimebalance kila upande licha ya Simba kubebwa na historia ya kufunga mabao mengi katika kipindi hicho kulinganisha na Yanga.

Katika mechi 20 ambazo zimezikutanisha timu hizo tangu Aprili 04, 2010 hadi Februari 14 2019 kila moja imeshinda michezo sita na kutoka sare mara nane zilipokutana ukiachilia mbali sare ya mabao 2-2 ya msimu huu katika mechi ya mzunguko wa kwanza.

Katika mechi hizo 20 ambazo zinajumuisha mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Simba iliwafunga Yanga bao 1-0 katika mechi tatu tofauti na kupata ushindi mwingine mnono wa mabao 2-1, 5-0 na 4-3.

Advertisement

Yanga katika mechi hizo 20, imeifunga Simba mara sita kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mechi tatu tofauti na ule wa bao 1-0 katika michezo mingine mitatu tofauti .

Tangu 2010, timu hizo zimetoka sare mara nane, zikipata suluhu katika michezo miwili na sare ya bao 1-1 katika michezo mitano na kutoka sare ya mabao 3-3.

Katika mechi hizo 20, mabao 43 yalifungwa huku Simba ikiongoza kwa kufunga mabao mengi zaidi ya Yanga, ikipachika mabao 22 wakati wapinzani wao hao wakipachika mabao 21.

Rekodi za karibuni Simba yatakata

Wakati Simba ikiongoza kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 68, pointi 11 zaidi ya Yanga yenye pointi 47 ikiwa kwenye nafasi ya tatu, rekodi za msimu huu zinaibeba zaidi Simba katika mchezo huo.

Katika mechi 26 ambazo Simba imecheza, imeshinda 22, imetoka sare mbili na kufungwa mara mbili huku ikipachika mabao 55 na kufungwa mabao 14.

Yanga yenyewe imecheza mechi 24, imeshinda 13, imetoka sare michezo minane na kufungwa miwili, katika mechi hizo imefunga mabao 29 na kufungwa 18.

Mechi tano za mwisho mambo yalikuwa hivi

Katika mechi tano za hivi karibuni kwenye Ligi Simba imeshinda michezo yote mitano kwa mabao 3-2 dhidi ya Azam, imeichapa KMC 2-0, imeifunga Biashara Mara mabao 3-1 na kutoa kipigo cha bao 1-0 kwa Lipuli.

Yanga imeshinda michezo miwili na kutoka sare mara tatu ya bao 1-1 na Polisi Tanzania, imesuluhu na Coastal Union na Tanzania Prisons na kushinda mabao 2-0 dhidi ya Alliance na matokeo kama hayo dhidi ya Mbao FC.

Katika mechi tano za karibuni, Yanga imefunga mabao matano kupitia kwa Tariq Seif, Ditram Nchimbi (2), Patrick Sibomana na David Molinga anayeongoza kwa kupachika mabao Yanga akiwa na mabao nane. Beki ya Yanga iliruhusu bao moja katika mechi hizo tano ambalo lilifungwa kipindi cha pili dakika ya 71 wakati washambuliaji wake wakifunga mabao matatu kipindi cha pili dakika ya 48, 79, 82 na mawili kipindi cha kwanza dakika ya 28 na 41.

Simba katika mechi hizo tano, imefunga mabao 10 huku mfungaji wake kinara, Meddie Kagere mwenye mabao 15 akipachika matatu sawa na Luis Miquissone, mengine yamefungwa na Deo Kanda, Erasto Nyoni, Francis Kahata na John Bocco. Safu ya ushambulijia ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu katika mechi hizo tano za karibuni imekuwa moto zaidi kipindi cha pili ambapo kati ya mabao 10 waliyofunga, sita yamefungwa kipindi cha pili dakika ya 72, 71, 72, 88, 69 na 61 na manne kipindi cha kwanza dakika ya 16, 9, 23, 35 japo wamefungwa mabao matatu dakika ya 06, 50 na 72.

Nyota Simba, Yanga watabiri mshindi

Licha ya mechi ya Simba na Yanga kutotabirika, baadhi ya nyota wa zamani wa timu hizo kongwe nchini wamesema mshindi wa Jumapili atapatikana kwa mambo matatu.

“Itetegemea na wachezaji walivyoamka siku hiyo, mbinu za makocha na timu itakayofanya makosa ya kizembe,” alisema nyota wa zamani wa Simba, Malota Soma.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...