Search This Blog
Sunday, March 8, 2020
Rais wa Uturuki: Hatutosita kaunza upya operesheni iwapo jeshi la Assad litakiuka makubaliano
Rais wa Uturuki azungumza kuhusu makubaliano ya kusitishwa mapigano Idlib na kusema kuwa jeshi lipo tayari iwapo makubaliano yatakiukwa.
Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kwamba jeshi la Uturuki halitosita kuanza upya operesheni yake iwapoa jeshi la Assad litakiuka makubaliano Idlib.
Kwa mara nyingine rais Erdoğan amekumbusha kuwa kamwe Uturuki haina lengo la kuhujumu ardhi ya Syria katika operesheni zake.
Kwa mujibu wa rais Erdoğan watoto na wanawake ndio waathirika waliomstari wa kwanza katika mapigano yanayoendelea nchini Syria.
Rais Erdoğan amesema kuwa ameshangazwa kwa kutoona yeyote anaekemea madhila yanayowakumba watoto na wanawake katika vita na mauji ya Syria.
Hayo rais Erdoğan ameyazungumza katika hotuba yake aliotoa katika hafla ilioandaliwa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake.
Siku kuu hiyo nchini Uturuki imeandaliwa kwa kuwaenzi wanawake waliojitolea kulilinda taifa la Uturuki.
Hakuna yeyote aliezungumza kuhusu wanawake wanaotaabika miongoni mwa wahamiaji zaidi ya 100 000 wanaonyanyaswa wanaotaka kwenda katika mataifa ya Ulaya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment