Rais Donald Trump amefanyiwa vipimo na kugundulika kuwa hajaambukizwa virusi vya corona. Daktari wake Sean Conley amethibitisha taarifa hizo, na kusema rais Trump aliamua kufanyiwa vipimo siku ya Ijumaa baada ya kukaribiana na afisa wa Brazil ambaye aliambukizwa COVID-19.
Rais Trump ametangaza kuziongeza Uingereza na Ireland katika orodha ya nchi ambazo abiria wake wamezuiliwa kuingia Marekani.
Hapo awali marufuku hiyo iliwahusu abiria wa mataifa ya Ulaya. Huko Uhispania serikali inapanga kuwafungia raia wake karibu milioni 46 kuanzia kesho Jumatatu kama sehemu ya mpango wa hali ya dharura wa siku 15 kukabiliana na mripuko.
Ufaransa imeyafunga maduka, migahawa na maeneo ya burudani kuanzia leo Jumapili huku raia wakielezwa kubakia nyumbani huku kesi za maambukizi zikiongezeka mara mbili katika muda wa saa 72.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment