Muungano wa Ulaya umepiga marufuku wasafiri kutoka nje ya muungano huo kwa siku 30 katika hatua ambayo haikutarajiwa ya kufunga mika yake kufuatia mzozo wa coronavirus.
Hatua hii inayahusu mataifa 26 wanachama wa EU pamoja na Iceland, Liechtenstein, Norway na Uswiss. Raia wa Uingereza hawataathiriwa na hatua hiyo.
Marufuku hiyo inatolewa huku idadi ya vifo vinavyotokana na mlipuko wa coronavirus ikiendelea kuongezeka katika nchi za Italia, Uhispania na Ufaransa imeweka masharti kali ya kuzuwia shughuli za umma na kuwataka raia wasalie majumbani mwao.
Ulaya imeathirika vibaya na virusi ambavyo vimewauwa watu 7 ,500 duniani.
Wakati huo huo mashindano ya kombe la Euro 2020 limeahirishwa kwa mwaka mmoja.
Virusi vya corona vimewaathiri zaidi ya watu 185,000 kote duniani, kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO).
Marufuku ya safari itaathiri raia wote ambao sio wanachama wa EU wanaotembelea nchi za Muungano huo, isipokua wakazi wa muda mrefu, wanafamilia kutoka nchi wanachama wa Muungano huo na wanadiplomasia, wafanyakazi wa mipaka na wahudumu wa afya na watu wanaosafirisha bidhaa.
Kwa kawaida matembezi ya raia kutoka za eneo la Schengen wamekua na uhuru wa kusafiri katika mataifa ya Muungano wa Ulaya bila pingamizi.
Lakini katika siku za hivi karibuni nchi nyingi zimeweka masharti ya kuingia kwenye mipaka yake ili kuzuwia kusambaa kwa coronavirus.
Hii imeifanya tume ya muungano huo kupendekeza kuwa Muungano huo kuchukua hatua katika mtindo wa pamoja na kuweka masharti ya kuingia katika muungano mzimakutokana na ombi la rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Hatua zilikubaliwa katika kiao kilichofanyika kwa njia ya video baina ya viongozi wa EU siku ya Jumanne mchana na sasa zitatakiwa kuekelezwa na nchi wanachama.
"Walisema watafanya hivyo mara moja ,"alisema Kamishna mkuu wa EU Ursula von der Leyen katika mkutano na waandishi wa habari. "Hili ni jambo zuri, ili tuwe na mbinu ya pamoja ya kushughulikia mipaka''
Uingereza na Jamuhuri ya Ireland - ambayo ni sehemu ya EU lakini ni mwanachama wa Schengen - itakaribishwa kujiunga na hatua hiyo.
Ilikua ni muhimu kwa muungano wa EU " kuwa wazi " kuhusu wkufungwa kwa mipaka ya ndani , Bi Von der Leyen aliesma , kwasababu "watu wengi walikua wamekwama".
Nchini Ufaransa, raia wanoondoka majumbani mwao lazima wabebe waraka unaoelezea ni kwa nini, huku nchi hiyo ikiwa imeweka faini ya €135 ($150; £123) kwa yeyote atayekiuka amri ya kutotembea bila sababu.
Rais Emmanuel Macron awali aliwaamuru watu kubaki majumbani mwao na waende nje tu pale wanapoenda kufanya majukumu muhimu. Bwana Macron alisema: "Tuko vitani... hatupambani na jingine lolote lile wala nchi yetu wenyewe. Lakini adui yuko hapa, haonekani, hawezi kuguswa ... na anasonga mbele."
Nchini Uingereza, idadi ya vifo imefikia watu 71, na watu wamekua wakiambiwa waepuke matangamano ya kijamii, watu kufanyakazi nyumbani ikiwa wanaweza na kuepuka safari za kigeni zisizo muhimu.
Waziri Mkuu Bois Johnson Jumatatu aliwataka watu waepuke kwenda kwenye maeneo kama vile baa,vilabu vya pombe na migahawa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisem Ufaransa inapambana na adui asiyeonekana wala kuguswa alipokua akitoa maagizo ya udhibiti wa coronavirus
Wakati huo huo mshauri mkuu wa serikali wa masuala ya kisayansi amesema ''itakua na matokeo mazuri'' kama watu 20,000 au wachache zaidi watakufa kutokana na virusi vya coronavirus nchini Uingereza.
Idadi ya vifo katika nchini ya Uhispania imeongezeka kutoka watu 2,000 hadi 11,178. Mamlaka nchini humo zimeweka marufuku ya matembezi na shughuli zisizo za lazima kwa rais wa nchi hiyo milioni 47.
Italia sasa ni nchi ya pili iliyokumbwa na mlipuko baada ya Uchina. Kumekuwa na masharti makali ya kuzuwia mikusanyiko ya umma ili kujaribu kusitisha usambaaji waq virusi.
Masharti yalitekelezwa kwa mara ya kwanza kaskazini mwa nchi, kabla hayajatekelezwa kitaifa.
Serikali imewataka watu milioni 60 wa Italia kubakia majumbani mwao pale inapowezekana.
Mtu wa kwanza ajitolea kufanyiwa chanjo ya coronavirus
Wakazi wanaweza kutoka nje ya nyuma zao tu pale wanapokua na hitaji la dharura, kama vile kununua bidhaa muhimu na wanatarajiwa kutembea na kibali maalum kinachoelezea sababu ya safari yao.
Wanaokiuka amri hiyo wanakabiliwa na tisho la kutozwa faini ya dola 235 kwa kuvunja sheria au hata kufungwa jela kwa muda wa miezi mitatu.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment