
Dar es Salaam. Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amekutwa na virusi vya ugonjwa wa corona ambapo pia mechi kati ya timu yake na Brighton iliyotarajiwa kuchezwa wikiendi imeahirishwa.
Raia huyo wa Hispania, mwenye umri wa miaka 37 alisema kuwa aliamua kupimwa baada ya kujihisi vibaya lakini atarudi kazini mara tu atakaporuhusiwa kufanya hivyo.
Arsenal ilikuwa icheze na Brighton katika mechi ya ligi Jumamosi hii muda wa saa 11 jioni lakini Brighton ikatoa taarifa muda mfupi baada ya Arteta kugunduliwa ameambukizwa virusi vya ugonjwa huo hatari, ikitangaza kwamba mechi hiyo imeahirishwa.
Kufuatia hali hiyo iliyotokea klabu ya Arsena maarufu kwa jina la The Gunners wamefunga uwanja wao wa mazoezi na wafanyakazi wa klabu hiyo waliogusana na Arteta wamelazimika kujiweka karantini.
Klabu ya Chelsea nayo imetangaza mchezaji wake Callum Hudson Odoi amekutwa na virusi vya corona.
Licha ya kupatikana na ugonjwa huo Klabu ya Chelsea imesema kuwa callum anaendelea vyema na anatarajia kurudi katika uwanja wa mazoezi atakaporuhusiwa.
Wachezaji wote wa Chelsea waliogusana naye kikiwemo kikosi chote cha wachezaji 11, wafanyakazi pamoja na wakufunzi sasa watahitajika kujiweka karantini kwa kipindi cha siku 14, ilisema klabu hiyo.
Premier itafanya mkutano wa dharura na klabu zote siku ya Ijumaa ili kuzungumzia kuhusu mechi zinazotarajiwa kuchezwa.
No comments:
Post a Comment