Search This Blog

Thursday, March 12, 2020

Juventus inafanya mambo yake kwa Kane kimyakimya

WAKATI timu kibao zikipiga kelele kila kukicha juu ya kuhitaji saini ya straika wa Tottenham Hotspur, Harry Kane, Juventus kwa upande wake imeamua kufanya yake kimyakimya ikisubiri timu hizo zijipindue tu imalize shughuli.

Unaambiwa staili ileile iliyotumika kumnasa Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid ndiyo itatumika kumaliza ishu ya usajili wa Kane anayefukiziwa pia na Manchester United na Real Madrid.

Juventus inajua kuwa sababu kubwa ya Kane kutaka kuondoka Spurs ni mataji, na inao uhakika inaweza kumhakikishia medali kama akikubali kutua Turin wakati wa kiangazi na kuipotezea Man United ambayo haipo vizuri sana katika siku za karibuni.

Mbali na Kane, Juventus pia inamfuatilia kwa karibu straika wa Inter Milan aliyepo kwa mkopo Paris Saint Germain, Maura Icardi, Gabriel Jesus wa Manchester City na Timo Werner wa RB Leipzig.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...