Search This Blog

Tuesday, March 10, 2020

Mbatia atoa msimamo sekta ya michezo

By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema michezo inapaswa kuingizwa katika mfumo rasmi wa elimu ili Taifa lipige hatua katika sekta hiyo.

Akizungumza na wahariri wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), alipotembelea ofisi zake zilizopo Tabata, Relini Dar es Salaam jana, Mbatia alisema michezo ikiingizwa kwenye mifumo rasmi kwa vitendo, vifaa vikiwepo shuleni na kujenga mfumo wa kubaini vipaji vya aina mbalimbali, Taifa litapiga hatua katika sekta hiyo muhimu kwa ajira ulimwenguni.

“Suala la michezo ni nyeti kwa sababu linanyanyua uchumi wa nchi. Itaingizia mapato. Naona nchi nyingine za Afrika wanavyowezesha katika masuala ya kimichezo.

“Michezo licha ya kipato cha mmojammoja, inaingiza vipato vya wengi zaidi kwa hiyo hili ni suala pana ambalo sisi katika NCCR Mageuzi tunalizungumzia katika kuwawezesha kupitia mfumo rasmi wa elimu waweze kupata vipaji na walimu waweze kuandaliwa vizuri,” alisema Mbatia.

Akisisitiza kuhusu kubaini vipaji, mbunge huyo wa Vunjo alisema, “kama mtu sekta yake ni ya michezo apelekwe kwenye michezo usije ukamlazimisha akaenda kwenye sekta ambayo sio ya kwake.”

Alisema licha ya kwamba michezo inaburudisha, kuleta jamii pamoja na masuala ya ajira, Taifa halina budi kuiangalia sekta hiyo kwa mapana yake. “Sisi Taifa, sera yetu ya michezo iko namna gani, kitaifa. Badala ya kushindana kwamba NCCR msimamo wake ni huu,”aliongeza Mbatia.

Advertisement

Aliwataka wanasiasa kuacha kuwatumia vijana katika kujiejengea umaarufu badala yake wawasaidie kujiendeleza kiuchumi na kuiendeleza jamii kwa pamoja.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...