Search This Blog

Monday, March 2, 2020

LIVERPOOL ,ENGLAND . INVINCIBLES. Ukilisikia neno hilo kwenye Ligi Kuu England basi moja kwa moja wanaohusika ni Arsenal.

Maana yake ni kwamba walicheza kwa msimu wote kwenye ligi hiyo bila ya kupoteza mechi hata moja. Hiyo ilikuwa msimu wa 2003-2004.

Msimu huu, Liverpool walikuwa na ndoto za kuvunja rekodi hiyo ya Arsenal ya kucheza msimu wote bila ya kupoteza. Lakini, Jumamosi iliyopita, ndoto hizo zilikatishwa na Watford, baada ya kuwachapa Liverpool 3-0 uwanjani Vicarage Road.

Liverpool walikuwa hawajapoteza mchezo wowote kwenye ligi msimu huu hadi kufikia mchezo huo wa 28, ambapo walikuwa wameshinda 26 na kutoka sare moja. Lakini, sasa rekodi yao imetibuliwa na hivyo kuwaaacha Arsenal pekee yao kwenye historia ya Ligi Kuu England kucheza msimu mzima bila ya kupoteza mechi hadi sasa.

Wako wapi mastaa wa Kikosi cha Kwanza cha Arsenal iliyocheza msimu wote bila ya kupoteza mechi kwenye Ligi Kuu England. Arsenal waliweka rekodi pia ya kucheza mechi 49 bila ya kupoteza, wakati Liverpool wao wameishia mechi ya 44 tu.

Hiki hapa kikosi cha Arsenal ya Invincibles ya msimu wa 2003-04 na mahali walipo, ambapo kocha wao, Arsene Wenger kwa sasa ni bosi wa Fifa.

Advertisement

Jens Lehmann, kipa

Lehmann ni kipa Mjerumani kipindi hicho akicheza kwenye kikosi cha Arsenal na baadaye alirudi hapo kufanya kazi kwenye benchi la ufundi chini ya Unai Emery. Lehmann iliondoka Arsenal baada ya kuwa kwenye benchi la ufundi la timu kwa miezi 12 chini ya Arsene Wenger. Kipa huyo aliguswa na kitendo cha kuondolewa, akisema lile kundi lote la Arsenal isiyoshindika halitakiwi kwenye timu hiyo. Kwa sasa Lehmann ni kocha msaidizi wa klabu ya FC Augsburg ya Ujerumani.

Lauren, beki wa kulia

Kipenzi cha mashabiki wa Arsenal. Beki huyo wa kulia alipendwa sana na mashabiki wa Arsenal na alikuwa kipenzi cha Kocha Arsene Wenger. Baada ya kuachana na soka kama mchezaji, staa huyo wa zamani wa Cameroon alijiingiza kwenye kazi ya kuchambua soka kwenye televisheni ya Sky Sports, lakini kwa upande wa soka la Hispania na amekuwa akifanya uchambuzi pia BBC na Eurosport huku akifanya kazi yake ya kuwa balozi wa Arsenal.

Ashley Cole, beki wa kushoto

Kwa wachezaji wote waliokuwa kwenye kile kikosi cha Arsenal hii, Cole hakuwekwa kwenye kitabu cha wakali hao kwa sababu ya kuhofia kuwatibua mashabiki wa Arsenal ambao walichukizwa na uamuzi wa beki huyo wa kushoto kuamua kutimkia Chelsea. Kwenye orodha ya wachezaji wa Arsenal ile, Cole aliendelea kucheza kwa muda kidogo akienda kutamba huko LA Galaxy kabla ya kurudi England kuichezea Derby Count iliyokuwa chini ya Frank Lampard. Kwa sasa amestaafu na yupo tu akifanya shughuli zake nyingine.

Sol Campbell,beki wa kati

Kutoka kujigamba yeye ni mtu mwenye akili ya mpira hadi kujiingiza kwenye masuala ya siasa akiwa Mbunge wa Conservative, Campbell maisha yake baada ya kujizulu soka yamekuwa matamu kweli kweli.

Beki huyo wa kati wa zamani huko Arsenal na England, alipiga sana kelele za kutokuwapo kwa makocha weusi kwenye Ligi Kuu England na kulalamika kitendo cha timu za ligi za juu kushindwa kumpa ajira licha ya kufanya vyema kwenye ligi za chini. Campbell kwa sasa ni kocha wa Southend United.

Kolo Toure,beki wa kati

Beki huyo wa zamani wa Ivory Coast, Kolo Toure alitimkia zake Manchester City kisha akaenda Liverpool. Kwenye kikosi cha Liverpool alikutana na Kocha Brendan Rodgers, ambaye wameelewana vyema na kufanya kazi kwa pamoja, ambapo alimchukua kwenda naye Celtic alikombadilisha kumfanya kocha wake msaidizi. Na baada ya kupata kazi Leicester City, Rodgers alirudi zake na Kolo England na kuwa msaidizi wake huko King Power.

Gilberto, kiungo mkabaji

Aliitwa Ukuta usionekana. Kiungo huyo wa Kibrazili, Gilberto, alikuwa moto kweli. Gilberto ameripotiwa pia kuwa na mchango mkubwa katika kumshawishi Fred aende kujiunga na Man United. Gilberto amekuwa akijihusisha pia na mradi wa Street Football League, huko Uingereza, ambao umejikita zaidi katika kuandaa mechi za hisani za soka kwa ajili ya kusaidia wasiokuwa na makazi huku akifanya kazi za ubalozi wa klabu ya Arsenal.

Patrick Vieira,kiungo wa kati

Kama ilivyo kwa Mikel Arteta, Vieira aliamua kujiunga na benchi la ufundi la Manchester City baada ya kuachana na maisha ya soka akiwa mchezaji na huko Man City alikuwa kwenye timu ya watoto. Kisha alienda kuinoa timu nyingine ya Man City, New York City FC huko kwenye Ligi Kuu Marekani na baada ya kuonekana kuwa vizuri, Vieira amepewa kazi ya kuinoa Nice na amekubali licha ya hapo awali kuhusishwa na mpango wa kwenda kumrithi Arsene Wenger huko Arsenal. Vieira bado anashikilia mikoba ya kuinoa OGC Nice ya Ufaransa.

Freddie Ljungberg,kiungo wa kulia

Ljungberg ni mchezaji pekee wa ile Arsenal ya Invincible, ambaye amerudi kwenye timu hiyo huko Emirates akiwa kocha wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 23. Kocha Ljungberg mechi yake ya kwanza kuisimamia Arsenal ya ilikuwa dhidi ya Brighton uwanjani Emirates wiki iliyopita.

Huko nyuma aliwahi kuwa kocha wa timu ya vijana chini ya miaka 15 kabla ya kwenda kujiunga kwenye benchi la ufundi la Wolfsburg ya Ujerumani akiwa kocha msaidizi kabla ya kuondolewa Septemba mwaka jana. Akachaguliwa kuwa msaidizi wa Unai Emery kabla ya kuinoa timu hiyo kama kocha wa muda na sasa amekuwa msaidizi wa Mikel Arteta.
Robert Pires,kiungo wa kushoto

Winga matata kabisa, Roberto Pires alikuwa mmoja waliokuwa wakipanga benchi la ufundi huko Arsenal hadi hapo mwishoni mwa msimu 2017 ambapo alionekana kuwa tayari kutaka nafasi kwenye benchi la ufundi la Arsenal chini ya kocha Emery. Kwa sasa Pires anafanya zaidi kazi za ubalozi wa timu hiyo akihusika kwenye kutambulisha jezi mpya za timu hiyo. Bado anafanya shughuli za ukocha huko Arsenal.

Dennis Bergkamp,straika

Bergkamp alijiweka mbali na masuala ya ukocha na alikataa ofa ya kutoka Arsenal kwenda kuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu hiyo na kuamua kupumzika na familia yake baada ya kustaafu soka.

Lakini, baada ya Mdachi huyo aliingia kwenye ukocha, amekuwa sehemu muhimu kwelikweli katika maendeleo ya klabu ya zamani ya Ajax ya huko Uholanzi akishiriki vyema kutengeneza makinda wa maana akiwa kocha msaidizi. Lakini, alifutwa kazi huko Ajax, Desemba 2017. Baadaye alienda kufanya kazi ya kujitolea huko Almere City.

Thierry Henry, mshambuliaji

Kinara wa muda wote wa mabao huko Arsenal. Henry amejengewa hadi sanamu nje ya Uwanja wa Emirates, lakini aliamua kuachana na kazi ya kunoa kikosi cha umri chini ya miaka 18 huko Arsenal na kwenda kufanya kazi ya kuchambua soka kwenye televisheni ya Sky Sports.

Henry kisha akajiunga na Ubelgiji akiwa msaidizi wa kocha Roberto Martinez na walifanikiwa kuisaidia timu hiyo kushika nafasi ya tatu kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 huko Russia. Alipata kazi ya kuinoa Monaco akapigwa chini. Kwa sasa ni kocha wa Montreal Impact ya Marekani.

Wakianzia benchi

Beki, Martin Keown mchambuzi wa soka BBC na BT Sport huku akiwa na kolamu yake pia kwenye Sportsmail, wakati Ray Parlour kwa sasa ni mchambuzi wa soka kwenye talkSPORT na amekuwa akitangaza pia mechi za soka kwa kushirikiana na Alan Brazil. Mbrazili, Edu amekuwa akifanya kazi na Timu ya Taifa ya Brazil akiwa meneja na aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Iran chini ya Carlos Quieroz kwenye Kombe la Dunia 2014 kabla ya sasa kuwa mkurugenzi wa soka huko Arsenal.

Gael Clichy, aliyekuwa kinda wa wakati huo bado anacheza hadi sasa akiwa kwenye klabu ya Istanbul Basaksehir ya Uturuki, huku Jose Antonio Reyes, ni marehemu, alifariki kwenye ajali ya gari.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...