
LONDON, ENGLAND. UONGOZI wa Ligi Kuu England umewakataza wachezaji wa ligi hiyo kushikana mikono kwa sababu ya hofu ya kirusi cha corona ambacho kimekuwa kikiisumbua dunia kwa sasa.
Kwa mujibu wa taarifa ya uongozi wa ligi hiyo, utaratibu wa wachezaji wa timu iliyonyumbani kupita mbele ya wageni utabaki pale pale, lakini mabadiliko yatakuwa ni kwamba safari hii hawatashikana mikono.
Wiki iliyopita kocha wa Newcastle United, Steve Bruce alidai kuwa klabu yake imeacha utaratibu wa kusalimiana kwa kushikana mikono asubuhi, huku David Moyes wa West Ham akidai kuwa wachezaji wake watapeana tano badala ya kushikana mikono.
Southampton nayo imekataza wachezaji kusaini vitabu vya kumbukumbu vya mashabiki na kupiga nao picha, lakini wakati hilo likiendelea EPL inajiandaa kuanza kucheza mechi zake bila mashabiki.
No comments:
Post a Comment