Search This Blog
Tuesday, March 10, 2020
Hukumu Ya Freeman Mbowe na Vigogo Wengine CHADEMA ni Leo Mahakama Ya Kisutu
Mahakama ya Kisutu leo March 10, inatarajia kutoa hukumu kwa Viongozi wa CHADEMA wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi mahakamani hapo.
Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, vigogo hao wanakabiliwa na mashtaka 13, wakituhumiwa kwa uchochezi, katika kesi iliyoanza kusilikizwa Machi 7, 2018 na Hakimu ambaye sasa ni Jaji, Wilbard Mashauri.
Mbali na Mbowe, wengine ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji na Katibu Mkuu wa sasa, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu visiwani, Salum Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na mbunge, Halima Mdee.
Wabunge wengine ni Esther Matiko, Esther Bulaya, Mchungaji Peter Msigwa na John Heche. Katika kesi hiyo, baadhi ya washtakiwa waliwekwa mahabusu kwa miezi mitatu kutokana na kukiuka masharti ya dhamana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment