Search This Blog
Tuesday, March 10, 2020
Aston Villa Ya Mbwana Samatta Yapigwa 4-0 EPL
KWENYE mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa King Power kati ya Leicester City dhidi ya Aston Villa usiku wa kuamkia leo mambo yamekuwa mazito kwa Villa ya Mbwana Samatta baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-0.
Harvey Barnes alianza kuitungua Villa dk ya 40 Jamie Vardy alipachika bao la pili dakika ya 63 mkwaju wa penalti kabla ya kurejea tena kambani dakika ya 79 huku mkwaju wa mwisho ukipachikwa na Barnes tena dk ya 85.
Aston Villa haikuambulia bao kwenye mchezo huo ambao mabeki walionekana kupoteana mwanzo mwisho.
Matokeo hayo yanaifanya Villa kuwa nafasi ya 19 ikiwa imecheza mechi 28 kwenye msimamo ikiwa na pointi 25 na Leicester City kuwa nafasi ya tatu na pointi 53 ikiwa imecheza mechi 29
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment