Uhispania jana imetangaza vifo vipya 394 vilivyosababishwa na virusi vya corona, na kufanya jumla ya vifo vilivyotokea nchini humo kufikia 1,720.
Idadi hiyo inalalifanya taifa hilo kuwa la pili kwa idadi ya vifo, baada ya Italia. Idadi hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 30 ikilinagnishwa na siku moja iliyopita.
Na idadi ya waliothibitishwa kuwa na virusi imeongezeka kutoka watu 3,646, sawa na asilimia 14.6, hadi watu 28,572.
Wizara ya afya ya Uhispania imeonya kwamba maambukizi yataongezeka zaidi kwa siku zijazo.
Upo wasiwasi wa kuwepo kwa mrundikano wa watu katika hospitali nyingi nchini humo katika wakati huu ambao watu walio katika uangalizi wa wagonjwa mahututi ikifikia 1,785.
Hapo jana Waziri Mkuu wa Uhisapania Pedro Sanchez alisema mripuko huo ni kati ya hali mbaya zaidi ulimwenguni, na itaendelea kuzorota zaidi.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment