Search This Blog

Sunday, March 22, 2020

Uingereza: Walio katika hatari wajiweke karantini

Uingereza imewaambia watu takribani milioni 1.5 ambao wapo hatarini kupatwa na maambukizi kujitenga kwa miezi mitatu kwa lengo la kujaribu kujiepusha na maambukizi ya virusi vya corona.

Miongoni mwa hao ni wenye saratani ya damu, magonjwa sugu ya mfumo wa upumuaji na waliofanyiwa upandikizwaji wa viungo.

Taarifa ya serikali imesema, shirika la huduma za afya la Uingereza NHS litawapelekea taarifa ya kimaandishi watu hao katika kipindi kifupi kijacho, na kuwafahamisha hatua mahususi za kufuatwa.

 Chama cha waandishi habari nchini Uingereza kimesema takribani watu 240 hadi sasa wamefariki dunia kutokana na mripuko huo.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amenukuliwa akisema serikali itachukua hatua ambazo hazijawahi kushuhudiwa, iwe katika amani au vita lakini ni za lazima.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...