Search This Blog
Wednesday, March 25, 2020
Hatima ya Meya Iringa kujulikana leo
Baraza la madiwani Iringa mjini litakutana leo Machi 26, 2020 huku kukitarajiwa maamuzi ya kumvua umeya, Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe.
Barua iliyotolewa na mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa hiyo, Hamid Njovu kwenda kwa Kimbe imemtaka kufika bila kukosa.
Machi 2 mwaka huu Kimbe alikiri kupokea barua kutoka kwa Njovu akitakiwa kujibu tuhuma zinazomkabili ndani ya siku tano.
Kimbe alisema anakabiliwa na tuhuma za mashtaka manne ambayo ni matumizi mabaya ya madaraka, matumizi mabaya ya rasilimali za halmashauri, mwenendo mbaya au ukosefu wa adabu na kushiriki vitendo vya rushwa.
Kimbe kupitia akaunti yake ya Twitter ameeleza kuwa alifungua kesi mahakamani kupinga hatua zinazochukuliwa na baraza la mawaziri na hukumu ilitakiwa kutoka Machi 27 ila ameshangazwa na kesho kuitwa kikaoni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment