Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa kushirikiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kipindi hiki cha kukabiliana na virusi vya Corona.
Josep Borrell ametoa mwito huo jana Jumatatu mjini Brussels na kuongeza kuwa, umoja huo unajiandaa kutuma misaada ya kibinadamu yenye thamani ya yuro milioni 20 hapa nchini Iran na Venezuela ndani ya wiki chache zijazo.
Kadhalika amesema EU inaunga mkono suala la Iran kupewa mkopo na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) kutokana na hali ngumu inayopitia nchi hii iliyosababishwa na vikwazo vya Marekani.
Mapema mwezi huu, Benki Kuu ya Iran iliiandikia barua IMF, ikiomba mkopo wa dharura wa dola bilioni 5 kwa ajili ya kupambana na Corona, hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Jamhuri ya Kiislamu kuomba mkopo tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment