Search This Blog
Monday, March 23, 2020
ATCL yasitisha safari zake za nje ya Tanzania
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuanzia Machi 25, 2020 litasitisha safari zake za nje ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na virusi vya corona.
Kwa mujibu wa taarifa ya ATCL iliyotolewa leo Jumatatu Machi 23, 2020 inaeleza kuwa safari hizo ni Entebe(Uganda), Bujumbura(Burundi), Hahaya(Comoro), Lusaka(Zambia) na Harare (Zimbabwe).
Kampuni hiyo imesema haitarejesha fedha badala yake abiria wote wenye tiketi katika safari zilizositishwa wanatakiwa kuwasiliana na ofisi za kampuni hiyo au wakala wa safari za ndege kwa ajili ya taratibu za kubadilisha tiketi hizo ili zitumike baadaye katika safari zao bila makato.
“Tumesitisha kwa sababu ya matamko na maagizo ya serikali mbalimbali katika nchi tunazofanya safari zetu, matamko hayo ni kufunga mipaka na kupunguza mwingiliano kwa sababu ya corona,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ACTL, Ladislaus Matindi.
“Tutarudisha safari hizo hali itakapoturuhusu. ATCL itaendelea kutoa huduma za ndani japo kwa kupunguza miruko katika baadhi ya vituo kutokana na upungufu wa abiria kipindi hiki cha tahadhali nyingi.”
Matindi ameahidi kampuni hiyo kuendelea kujali usalama na afya za wafanyakazi, abiria na wateja kwa kupuliza dawa, kusafisha kwa dawa maalumu ndani ya ndege na mikono.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment