Wakati Waziri wa Ujenzi, Isack Kamwelwe akiahidi daraja la Kiyegeya barabara ya Morogoro-Dodoma lililosombwa na maji kuanza kutumika kuanzia saa 4:00 usiku wa kuamkia leo, nauli za mabasi zimepanda.
Nauli zilizopanda ni Dar es Salaam kwenda Dodoma kupitia njia ya Iringa.
Daraja hilo lililopo Gairo linalounganisha mikoa ya Dodoma na Morogoro lililosombwa na maji juzi saa 9:00 alasiri kufuatia mvu zinazoendelea.
Juzi kabla ya Serikali kufunga barabara hiyo mamia ya abiria na magari yalikwama eneo hilo huku baadhi wakilazimika kutumia njia mbadala.
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini nauli kutoka Dar kwenda Dodoma kupitia Iringa ilikuwa Sh40,000 kutoka Sh22000 kwa basi daraja la kawaida; Sh28,000 hadi Sh45,000 daraja la kati; na Sh50,000 kutoka Sh35,000 daraja la maalumu (VIP) kupitia njia ya Iringa.
Umbali wa kutoka Dar-Iringa hadi Dodoma ni takriban kilomita 760, huku Dar-Moro hadi Dodoma ni kilomita 454.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment