Search This Blog

Monday, March 23, 2020

CHADEMA yasitisha mikutano yote ya chama


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, ametangaza kuahirisha mikutano yote ya chama hicho iliyopangwa kuanza Aprili nne mwaka huu.

Akizungumza wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mbowe amesema hatua hiyo ina lengo la kuepuka mikusanyiko inayoweza kusababisha maambukizi ya virusi vya corona.

Mbowe ametumia mkutano huo kuiomba serikali kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya mapambano dhidi ya virusi vya corona na si kutegemea fedha pekee zilizotolewa baada ya kuahirishwa kwa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu.

Pia ameshauri hospitali zote za mikoa nchini ziwezeshwe, ili ziweze kuwahudumia wagonjwa wa homa ya corona pindi wanapothibitika.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...