Search This Blog

Tuesday, March 3, 2020

Barcelona kuwatumia Vidal, Semedo kumnasa Martinez

BARCELONA imepania kuimarisha safu yake ya ushambuliaji katika usajili wa majira ya kiangazi na straika wa Inter Milan, Lautaro Martinez, ndiyo anaongoza orodha ya wachezaji ambao wanasakwa na miamba hiyo Nou Camp.

Ili kumnasa Martinez, Barcelona imeweka mezani ofa ya pesa taslimu Euro 70 milioni, pamoja na kuwatoa chambo wachezaji wawili wa timu hiyo ambao kiungo Arturo Vidal pamoja na beki wa kulia Nelson Semedo.

Mkataba wa Martinez unakipengele kinachosema kuwa timu yoyote inayomtaka straika huyo inatakiwa kukamilisha usajili wake kati ya Julai 1 hadi Julai 15 mwaka huu kwa dau la Euro 111 milioni.

Dau hilo ni kubwa sana kwa Barcelona na ndiyo maana imeamua kuwajumuisha Vidal na Semedo katika ofa yake, ikiamini kuwa uwepo wao utaishawishi Inter Milan kulegeza masharti na kupokea Euro 70 milioni.

Juzi Jumapili Barcelona ilipata kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Real Madrid na sasa wameona mapungufu yao.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...