
LAS VEGAS, MAREKANI . BONDIA Deontay Wilder alitumia Dola 60,000 kutengeneza vazi ambalo alilivaa wakati akiingia kupambana na Tyson Fury katika pambano la uzito wa juu duniani ambalo alichapwa kwa TKO katika raundi ya saba.
Kinachostaajabisha, licha ya kutumia pesa ndefu kutengeneza vazi hilo, lakini Wilder analalamika kuwa uzito wake ulichangia kupigwa katika pambano hilo lililofanyika Jumapili asubuhi katika Ukumbi wa MGM Grand Arena, Las Vegas, Marekani.
Vazi hilo la jeusi lililokuwa na mambo mengi ambayo yalilenga kutengeneza hofu kwa Fury, lilibuniwa na wabunifu wawili Cosmo na Donato ambao walikunja Dola 60,000 kwa kazi hiyo.
Wakati, Walder akilalamikia kuponzwa na vazi hilo, Promota wa Anthony Joshua, Eddie Hearn na yule wa Fury, Frank Warren wamemshangaa bondia huyo kwa kuja na sababu za kitoto kujitetea baada ya kula kichapo.
No comments:
Post a Comment