Search This Blog
Wednesday, February 12, 2020
Umeme chanzo cha moto soko la makoroboi
Na James Timber, Mwanza
Takriban vibanda 60 vya wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu machinga kutoka soko la Makoroboi jijini hapa vimeteketea kwa moto kutokana na hitilafu ya umeme.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dk. Philis Nyimbi alieleza kuwa Moto huo ulitokea jana saa tisa usiku huku juhudi za zimamoto zikisaidia kudhibiti madhara makubwa zaidi.
Nyimbi amewataka machinga ambao wamekubwa na janga hilo kuwa wavumilivu huku serikali ikiwa na jitihada za ufumbuzi wa haraka ili wanawake Vijana na walemavu waweze kurejeshewa mikopo yao, ambayo itasaidia kuendeleza biashara kama awali.
"Ninawaomba kuchangamkia fursa iliyotangazwa na halmashauri ili kuhakikisha wanaunda vikundi ili kupatiwa mikopo isiyokuwa na riba ili kuendelea na biashara zao na kufikia ndoto za kuwa wanyanyabiashara wakubwa," amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Machinga Taifa Ernest Masanja aliiomba serikali kuwaangalia wahanga wa janga hili kwa jicho la tatu maana wengi wao wanamikopo benki na kwenye Taasisi mbalimbali ili kupata mitaji haraka na kuendelea na biashara zao.
Hata hivyo, Amina Swalehe muhanga wa tukio hilo alieleza kuwa kwa Sasa haelewi anaanzia wapi kutoka na Mali yake yenye thamani ya milioni 5 kuteketea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...



No comments:
Post a Comment