Wakati ikiendelea kukosa huduma za mawinga wake wapya Luis Miquisone na Shiza Kichuya, Simba itashuka katika Uwanja wa Uhuru leo ikiwa na lengo la kuvuna pointi tatu dhidi ya 'Maafande' wa Jeshi la Polisi Tanzania ili kufikisha pointi 50 kuelekea 100 walizolenga kuzifikia msimu huu.
Hadi sasa Simba ina pointi 47 ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara, na mechi hiyo ya leo ni ya kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo yenye timu 20.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alimwambia mwandishi wetu kuwa lengo la klabu hiyo ni kuandika rekodi mpya kwa kuwa timu ya kwanza kufikisha pointi 100.
"Simba ni timu ya rekodi, tunataka ubingwa na ponti 100, kesho [leo] tunataka kufikia nusu ya lengo, hakuna timu iliyowahi kufikisha pointi 100," Manara alisema.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu, Simba watashuka uwanjani katika mechi hiyo wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union, wakati Polisi Tanzania iliwafunga JKT Tanzania bao 1-0, kwenye mchezo ambao ulimalizika siku ya pili kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment