Search This Blog

Friday, February 7, 2020

Nyota hawa kumbe hawaachi kitu bana

By Rhobi Chacha

MUZIKI wa Bongo Fleva kwa upo kati kwa kati tofauti na miaka michache iliyopita. Hilo halina ubishi. Wapo wanamuziki wanaofanya poa kwa mfano kina Diamond Plutnumz, Alikiba, Aslay, Vannesa Mdee, Marioo, Ommy Dimpoz, Jux, Weusi na wengine kibao tu.

Ukiachana na Bongo Fleva, mastaa wa Bongo Movie nao hawakpo nyuma kupambana kufanya mambo ili kuvuna mkwanja wa maana. Lakini, kuna wasanii wenyewe kila kona wapo kutokana na kujaaliwa vipaji vya uhakika. Yaani ukienda kwenye muziki wapo na huku kwenye filamu pia wamo.

Hapa Mwanaspoti linakuletea orodha ya wasanii wa Bongo Flava ambao wamejikita kwenye sanaa ya maigizo na sasa wanabamba katika tamthilia zinazotamba.

Nandy ni msanii wa Bongofleva, amewahi kutamba na nyimbo tamu zilizowashika mashabiki wa muziki huo ambazo ni, Kivuruge, Ninogeshe, Aibu, Wasikudanganye, Kiza Kinene na nyingine nyingi. Kwa sasa anafanya yake katika kuigiza tamthilia ya Huba inayorushwa DSTV. Anafanya vizuri kutokana na mvuto wake pindi anaponekana kwenye igizo hilo.

Nandy anasema uigizaji ulikuwa ndoto yake kabla hata hajaanza kuwa na wazo la kufanya muziki, hivyo kwa sasa anaona ndoto yake imetimia ya kuigiza.

Advertisement

Anafahamika zaidi kwenye Bongo Fleva kwa nyimbo zake kama vile ‘Utamu’, ‘Ona’, ‘Amezoea’, ‘Nilegeze’ na nyingine.

Lulu Diva kwa sasa anafanya mambo makubwa kwenye tamthilia ya Rebecca. Naye anasema amegundua tamthilia zinalipa kuliko muziki anaoufanya japo hajaacha, lakini ameamua kuuweka pembeni kwa muda.

GIGY MONEY

Gift Stanford ndio jina lake halisi. Ghafla tu aliibuka na bonge la ngoma la Nampa Papa kwenye Bongo Fleva. Akanogewa na kutoa single nyingine ya Shoga. Akazoea na kutoa kazi nyingine nyingi. Pia, aliwahi kuwa Video Queen kwenye nyimbo za Siachani Nawe (Baraka Da Prince) na Bishoo (Quick Racka ft Young Dee) na nyingine nyingi.

Gigy anaingia kwenye orodha ya wasanii waliojiingiza katika uigizaji, kwa sasa anaonekana kwenye tamthilia ya Kapuni.

Naye anasema amejiingiza katika uigizaji ili kuwaonyesha mashabiki zake kuwa ana kipaji kingine zaidi ya muziki mbali na kujiongezea kipato.

JOHN KITIME

Ni mwanamuziki mkongwe aliyetamba na Bendi za Mambo Bado Orchestra chini ya Tshimanga Kalala Assossa, Vijana Jazz na The Kilimanjaro ‘Wana Njenje. Pia, aliwahi kupita katika Bendi za Orchestra Makassy, TX Seleleka, Tancut Almasi Orchestra ya Iringa sambamba na Abdul Salvador, Kasaloo Kyanga na Kyanga Songa, kina Kawelee Mutimwana, Kalala Mbwebwe na majina mengine makubwa katika historia ya muziki Tanzania. Baadaye akatua Magoma Moto Sound na kwa sasa yuko na Wana Njenje.

Naye amejitosa kwenye uigizaji. Kitime anaigiza katika tamthilia ya Rebeka.

Jina lake halisi ni Hemed Suleiman. Msanii wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma za Usiniache, Mkimbie, Rudi Nyumbani, Imebaki Stori, Far away na nyingine nyingi.

Huyu ni mmoja kati ya wasanii wa filamu walioanza kitambo kugeukia tasnia hii, miongoni mwa filamu alizocheza ni Confusion akiwa na Lulu, Nisha, Diana Kimario pamoja na Bad Girl akiwa na Rose Ndauka na nyingine nyingi.

Kwa sasa anaonekana katika tamthilia ya Sarafu.

QUICK ROCKA

Ni msanii wa anatamba na ngoma za Falling, Bembeleza na Amina. Amejitosa kwenye tamthilia akitisha huko Kapuni ambako umebamba kinoma.

Anasema amejigeukia maigizo kutokana na kuipenda tangu akiwa mdogo pamoja na kumpa kipato na anakiri uigizaji umechangia kubadirisha maisha yake.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...